WATU 24 akiwamo dereva wa basi wamekufa papo hapo na wengine zaidi 30 kujeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso katika ajali ilyotokea Kijiji cha Kitumbi Wilayani hapa katika barabara kuu ya Segera - Chalinze.
Kwa mujibu wa habari za awali zilizopatikana na kuthibitishwa na maafisa wa polisi waliokuwepo katika eneo la ajali ni kuwa ajali hiyo ilitokea jana saa 8.50 mchana.
Walioshuhudia ajali hiyo muda mfupi uliopita walisema kuwa ajali hiyo ilihusisha basi la Kampuni ya Chatco iliyokuwa ikitokea Arusha kuelekea Jijini Dar es saalam lililovaana uso kwa uso na basi la Kampuni ya Mzuri Transport ambalo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Lushoto Mkoa wa Tanga na kwamba walishuhudia maiti nyingi zikiwa zimebebwa ndani ya lori.

Comments