Tuesday, February 02, 2010

Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar yakutana leo


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Aman Abeid Karume, akifunguwa mkoba kutowa kabrasha kwa ajili ya kufunguwa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichokutana leo katika Ukumbi wa CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Kushoto ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein. Photos by Amour Nassor (VPO)

Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar Dk. Mohamed Gharib Bilal kushoto na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho kulia, wakijadiliana jambo wakati wa kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichokutana leo katika ukumbi wa CCM Kisiwandui mjini Zanzibar.

Wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kupitia Umoja wa Vijana wa CCM Adila Hilal Vuai kushoto na Hawa Said Sukwa kulia, wakijadiliana jambo katika kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kinachokutana leo katika Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.

No comments:

RAIS SAMIA ATEMBELEA MABANDA YA MAONESHO YA NANENANE JIJINI DODOMA

Tarehe 8 Agosti 2025, viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma vilikua kitovu cha shughuli nyingi wakati wa Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa ya Nan...