Bomu Latelekezwa na Kupagawisha Wakazi wa Msasani Jijini


Wananchi wakishangaa bomu hilo lililobebwa na askari wa JWTZ likipelekwa sehemu maalumu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.


Jeshi la polisi kutoka kikosi cha usalama kwanza ambao walifika mapema kabisa kwa ajili ya kulinda usamala wa wananchi eneo hilo,huku wakiwasubiri wataalamu kutoka jeshi la wananchi Tanzania JWTZ kwa ajili ya kulifanyia uchunguzi zaidi.

Bomu lililotelekezwa likiwa nje ya ukuta wa mkazi mmoja wa msasani bonde la mpunga mapema jana.
------------

Wakazi wa Msasani Bonde la Mpunga eneo la Maandazi Road jijini Dar es Salaam,jana walikumbwa na hofu baada ya mtu asiyejulikana kutelekeza bomu kwenye kichochoro kimoja mtaani hapo.Afisa Mtendaji wa Mtaa huo Bi. Rose Temu, alisema kijana mmoja alionekana mtaani hapo akitafuta mtu wa kumuuzia bomu hilo kama chuma chakavu lakini wanunuzi walionesha wasiwasi kuwa huenda ni bomu ndipo kijana huyo aliamua kulitelekeza mtaani hapo.Kufuatia tukio hilo kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania,kikosi maalum cha kutegua mabomu, kilifika eneo la tukio na kuthibitisha kuwa ni bomu hatari na kulichukua na kuondoka nalo. Picha kwa msaada mkubwa wa Ahmed Michuzi

Comments