Friday, May 09, 2008

Ze Comedy nje ya EATV



KUNDI la sanaa za vichekesho nchini maarufu 'Ze Comedy' limemaliza mkataba wake wa miezi minane na Kampuni ya IPP na kwa sasa wasanii wake wana mapumziko kwa ajili ya kujipanga upya.

Kundi hilo lililojizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo wao wa 'The Comedy Show' limemaliza mkataba wake kupitia Televisheni ya East Africa na kwa sasa wanajipanga upya kwa ajili ya kutoa burudani zaidi kwa wapenzi wao.

Mkurugenzi mtendaji wa kundi hilo, Isaya Mwakilasa au 'Wakuvanga' alisema kwa muda usiopungua miezi minane walikuwa wakifanya kazi na IPP na kutokana na mkataba wao kumalizika kwa sasa wako katika mapumziko kwa ajili ya kujipanga upya.

"Tumefika kipindi sasa tunataka kufanya vitu tofauti na vya kipekee ili kuleta msisimko zaidi kwa mashabiki wetu na sasa tunataka kuja kivingine na kipekee ikiwa ni moja ya kuinua sanaa yetu hapa nchini," alisema Mwakilasa.

Naya kiongozi wa kundi hilo, Sekioni Gideon au Seki alisema yeye yupo pamoja na kundi hilo na kwa sasa watakua pamoja mapumzikoni kwa ajili ya kuja kitofauti zaidi na kuendeleza sanaa ya Tanzania ndani na nje.

Alisema mara baada ya kupumzika wao kama kundi wataamua kuweka mkataba na kituo chochote cha televisheni endapo watafikia muafaka ua kurudi katika kituo chao cha awali.

2 comments:

Anonymous said...

Wajomba hawa wanataka mshiko wa nguvu au wamenunuliwa na vituo vingine vya televisheni

Anonymous said...

Na hizi ni dalili tu za kuvunjika kwa kundi hili. They have to observe silence!!