Kivuko kipya kiwa katika matengenezo ya kukiungisha kama kinavyoonekana jana wakati Waziri wa Miundo Mbinu, Dk Shukuru Kawambwa alipofaya ziara ya ukaguzi wa ujezi wa kivuko hicho jijini Dar es Salaam, ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa Picha na Salhim Shao
Kivuko hicho kipya ambacho ni cha tatu cha Kigamboni, Dar es Salaam (Magogoni-Kigamboni) ambacho kimekuwa kwenye ujenzi kwa takribani miezi 15 sasa, kinatarajiwa kuanza kutumika rasmi Septemba mwaka huu.
Kwa sasa matengenezo ya kivuko hicho yamefikia asilimia 60 na mkandarasi wa kampuni ya Neue Ruhrorter Schiffswerft Gmbh ya Ujerumani ameomba kuongezewa miezi miwili aweze kukamilisha sehemu iliyobakia.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho Mei 22,2008 wakati Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alipokagua kivuko hicho Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ufundi wa Umeme wa wizara hiyo, John Ndunguru alisema kivuko hicho kitakachojulikana kama Magogoni-Kigamboni kikikamilika kitasaidia kuondoa kero ya usafiri Kigamboni.
Kivuko hicho ambacho kimeigharimu Serikali kupitia bajeti yake ya mwaka 2006/2007, Sh bilioni 8.8 kina urefu wa mita 74.5 na upana wa mita 17.44 na kina uwezo wa kubeba tani 500, yaani magari madogo 60 na abiria 2,000.
Comments