Monday, May 12, 2008

Kikwete amaliza mgogoro DRC, Uganda



RAIS Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa AU amewapatanisha Rais wa Uganda Yoweri Mseveni na Joseph Kabila wa DRC Congo katika mgogoro wa kugombania mpaka kati ya DRC na Uganda uliodumu kwa muda sasa.

Wakizungumza katika tamko la pamoja lililotiwa saini na mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Mbusa Nyamwisi na mwenzake wa Uganda Isaack Musumba viongozi hao kwa pamoja wamekubaliana kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa muda sasa.

Mgogoro huo ulianza Desemba 5 mwaka jana na waliitisha mkutano mwingine Desemba 12 hadi 15 mwaka huo huo Jijini Kampala wakisimamiwa na Rais Kikwete.

Marais Museveni na Kabila wamekubaliana kutoa ushirikiano muhimu kwa kamati ya pamoja inayoshughulikia mgogoro huo ili iweze kumaliza mgogoro huo.

Kuhusu visiwa vya Rukwanzi, wakuu hao wamekubaliana kimsingi kwa pamoja kuharakisha utawala wa pamoja wakati mchakato wa kuweka mipaka mipya ikiendelea.

Kwa upande wa usalama, wakuu hao wa nchi wamemtaka Kiongozi wa chama cha waasi cha LRA, Joseph Kony atie saini makubaliano ya mwisho ili kuharakisha mchakato wa amani wa Juba.

No comments: