Thursday, May 08, 2008

Chenge aanza ziara ya kudanganya watu kwao



Frederick Katulanda, Bariadi wa Mwananchi

LICHA ya aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kuwaomba radhi Watanzania kwa kudai kuwa Sh1.2bilioni anazodaiwa kuzificha katika Kisiwa cha Jersey ni vijisenti, jana alirudia tena usemi huo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Bariadi mjini.

Chenge aliwaambia wananchi waliofika kumsikiliza kuwa hawezi kunywa sumu na kuacha vijisenti vyake nyuma.

"Mnyantuzu, kamwe siwezi kunywa sumu ili nife na kuacha vijisenti vyangu nyuma..." alisema Chenge.

Akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Bariadi jana, Chenge alisema kuwa amesikitishwa sana kuzushiwa kuwa amefariki dunia na kusema kwamba hawezi kujiua na kuviacha vijisenti vyake.

Akizungumza kwa Lugha ya Kisukuma Chenge alisema: "Bhadugu bhane wakayomba niachile olwa sumu, bhadugu Mnyantuzu ong'wa sumu, oleka vijisenti byakwe?". Alikuwa ana maanisha kuwa, akiwa kama Msukuma Mnyantuzu hawezi kufa kwa kujiua na kuacha vijisenti vyake. Hebu cheki Mwananchi Uone mambozzz.

No comments:

TUZINGATIE UTU, SHERIA NA HAKI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA ULINZI WA RASILIMALI ZA TAIFA- DKT KIJAJI

  Na. Joyce Ndunguru, Morogoro. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Dkt Ashatu Kijaji (Mb) amewataka watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa W...