Simba wamsimamisha Kaduguda


Katibu Mkuu wa klabu ya soka ya Simba, Mwina Kaduguda amesimamishwa kwa muda usiojulikana kwa utovu wa nidhamu na kamati ya utendaji ya klabu hiyo iliyokutana juzi.

Habari za kuaminika toka ndani ya klabu hiyo na kuthibitishwa na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo zinasema kuwa, Kaduguda amesimamishwa na kikao hicho cha dharura kufuatia kitendo chake cha kumkashfu mfadhili wao mkuu.

Wajumbe wa kamati ya utendaji chini ya Mwenyekiti wake, Hassani Dalali wamedaiwa kufikia uamuzi kwa kinachodaiwa kushindwa kuendelea kuvumilia tabia za katibu mkuu wao huyo kwa muda mrefu.

Chanzo chetu cha habari kinasema kuwa, kwa muda mrefu katibu huyo amekuwa `akiharibu` lakini wenzake walikuwa wakimvumilia na kwa kitendo cha juzi cha `kumghasi` na kumkera mfadhili huyo wenzake wameamua kumgeuka.

``Yapo mambo mengi ukiambiwa yanafanywa na kiongozi huyu msomi huwezi kuamini, lakini wenzake wamekerwa na kuamua kumtia adabu, hadi hapo atakapoitwa kwenye mkutano mkuu ili kujitetea kwa adhabu aliyopewa,`` chanzo hicho kilisema.

Nipashe lilimtafuta mmoja wa viongozi wa klabu hiyo, ambaye alikiri kuwepo kwa maamuzi hayo, lakini akisema yalikuwa bado ayajabarikiwa mpaka kwanza kikao hicho kilichokuwa kikiendelea kimalizike. Picha ya Mrocky Mrocky

Comments