Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo jana jioni, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Festo Kang'ombe alisema kuwa Nangoro ambaye ni mgombea wa CCM ameibuka mshindi kwa kupata kura 21,506, wakati mgombea wa Chadema, Victor Kimesera alipata kura 12,561, mgombea wa Sauti ya Umma (Sau) Mashaka Fundi alipata kura 300 na mgombea wa PPT-Maendeleo, Juma Saini aliambulia kura 110.
Kang'ombe alisema kwamba idadi ya watu waliojiandikisha ni 74, 626, lakini waliokwenda kupiga kura ni 35, 261, idadi ambayo karibu ya nusu hawakwenda kupiga kura.
Hawa jamaa hawakuamini kabisa nini kimetokea (Picha zote za Mpoki Bukuku)
No comments:
Post a Comment