Friday, February 08, 2008

Bunge laahirishwa hadi saa 11 jioni

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limesitisha shughuli zake asubuhi hii hadi saa 11 jioni kufuatia uamuzi wa Rais Kikwete kuvunja baraza la mawaziri, uamuzi ambao automatically unaondoa uhalali wa kuwapo kikao cha bunge kutokana na upande wa serikali kutokuwapo

Akizungumza asubuhi hii Spika wa bunge hilo Samwel Sitta alisema ameamua kuchukua uamuzi huo kutoaka na kikao hicho kukosa upande wa serikali, hivyio kwa mujibu wa kanuni za bunge na taratibu zingine kikao hicho hakiwezi kufanyika.

"Nimepata taarifa kutoka kwa Rais Kikwete jana jioni akinieleza nia yake ya kuvunja bunge na kukubali, maombi ya mawaziri watatu kujiuzulu,"alisema Sitta.

No comments:

MAJALIWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA TEWW

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 25, 2025 ni mgeni rasmi katika kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu y...