Tuesday, February 26, 2008

Mazungumzo Kenya yasimama

MSIMAMIZI Mkuu wa mazungumzo ya pande mbili zinazovutana nchini Kenya, Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan amesimisha mazungumzo ya kutafuta amani.

Akizungumza na vyombo vya habari jana katika Hoteli ya Serena, jijini Nairobi alisema kamati yake imeamua kusimamisha mazungumzo hayo ili kujikita zaidi katika mashauriano na kila upande kwa kina, baada ya kuona hatua ya sasa haizai matunda.

Annan alisema kinachoonekana kwa sasa Kamati hiyo ya usuluhishi inahitaji kukutana na wakuu wa pande hizo mbilI, Rais Mwai Kibaki na Raila Odinga wa ODM kuliko kuendelea kuzungumza na wawakilishi wao, ambao mara kwa mara wamekuwa wakibadilika.

Alisema kwamba mazungumzo hayakusimamishwa bali wanatafuta njia muafaka zaidi, ambayo itakuwa ya kudumu.

"Bado hatujakata tamaa, tunachokitafuta ni suluhu ya kudumu kuliko ilivyo sasa," alisema.

No comments: