Mwenyekiti wa Chadema akihutubia mkutanoi mjini Kiteto leo.
Kapteni Komba aliyesshushwa jukwaani baada ya kudaiwa kuvamia mkutano wa Chadema.
Mbowe akishuhudia Helikopta ya Chadema iliyoujumiwa na kushindwakuruka toka Dodoma (Picha kwa hisani ya Chadema)
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimekodi helikopta itakayokisaidia kupambana na ile ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo katika kampeni za uchaguzi wa jimbo la Kiteto unaotarajiwa kufanyika kesho.
Helikopta hiyo iliyokodiwa kutoka Kenya , iliwasili kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, majira ya saa 3:20 asubuhi na kuanza kazi ya kupiga kampeni katika maeneo ya vijiji takribani vyote vilivyopitiwa na helikopta ya Chadema Juzi.
Mpaka jioni ya juzi taarifa zinaeleza kwamba CCM ilikuwa haijawasilisha baria ya maombi ya vibali kadhaa vikiwamo vya usjili, leseni ya Kapteni, mkataba wa kukodisha, kibali cha jeshi na maliasili, ingawa inaelezwa kwamba vibali hivyo vilitolewa uwanja wa ndege wakati ndege ikiwa imeshawasili.
Comments