Kalonzo aja Bongo

Musyoka: Usuluhishi Kenya umefikia hatua nzuri

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka amesema pande mbili katika mgogoro wa kisiasa nchini Kenya zimefikia hatua nzuri ya kuelekea kupata ufumbuzi kamili wa mgogoro huo.

“Hata jana (juzi)Rais Kibaki alikukutana na Koffi Annan na kujaribu kumwarifu vile hali ilivyo ya mazungumzo, kwa sasa hatujafikia maelewano ya mwisho mwisho, lakini hatua kabambe kusema kweli zimefanyika,” alieleza

Musyoka aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam akitokea Nairobi, Kenya ambapo alipokelewa uwanjani hapo na Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein.

Musyoka yuko nchini kwa ziara ya siku mbili kwa ajili ya kuleta ujumbe maalum kwa Rais Jakaya Kikwete kutoka kwa Rais Mwai Kibaki wa Kenya .

“Ujumbe ninao kutoka kwa Rais Kibaki wa Jamhuri ya Kenya kwa rafiki yetu, rafiki yake Jakaya Kikwete na huku tukileta pongezi nyingi sana tukijua kwamba kitendo ambacho kimetokea Kenya kimewakera sana ndugu zao Watanzania,” alidokeza. (Taarifa hii ya Ofisi ya Makamu wa Rais)

Comments

Anonymous said…
doorway edublogs legendi investigator administer workarounds volume digg wenger sara wolcott
masimundus semikonecolori