


Shughuli ya utiaji saini Ikulu asubuhi

Jamaaa kafuraaaahi kinoma huenda hakuwahi kupata generosity ya aina hii ya watu kuacha kazi na kisha kumpokea yeyetu.


Kama vile anamuambia ebwaana mambo vipi, unaonekana uko fiti Kanali, mwenzio mimi nilikimbia jeshi kule Marekani, vipi wwewe unaendelea.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi Condoreza Rice akiwasalimia wananchi alipoingia Ikulu Dar jana. Alikuwa na mvuto wa kipekee sijui kwakuwa ni bomba ama kw akuw ani black?

Askari wa Marekani akipita na mbwa ili kuhakikisha kuwa maeneo hayo ni salama kwa wazee kuingia.


Pichaa za juu ni Rais George Bush wa Marekani wakitia saini msaada mkubwa wa $ 700 Million kutoka serikali ya Marekani , Mkataba huo umekusudia kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa barabara tatu ambazo ni barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga,Tunduru Songea hadi Mbambabay na barabara ya Horohoro hadi Tanga na pia msaada huo mradi wa umeme katika mkoa wa Kigoma, mara baada ya kutia saini mlataba huo Rais Bush na Rais Kikwete walitembelea hospitali ya Amana iliyopo wilayani Ilala imepata mafanikio makubwa katika mradi wa mapambano dhidi ya Ukimwi ambapo pia umedhaminiwa na serikali ya Marekani.
Rais Bush anatarajia kwenda mkoani Arusha na kufanya shughuli ambako atalala na kurejea Dar es Salaam siku inayofuata na kuhitimisha Ziara yake nchini Tanzania na kuelekea Kigali nchini Rwanda. (Picha Mpoki Bukuku na Reuters)
No comments:
Post a Comment