Wednesday, February 06, 2008

Ripoti ya Richmond hiyo

MUHTASARI (EXECUTIVE SUMMARY) WA TAARIFA YA KAMATI TEULE ILIYOUNDWA NA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 13 NOVEMBA, 2007 KUCHUNGUZA MCHAKATO WA ZABUNI YA UZALISHAJI UMEME WA DHARURA ULIOIPA USHINDI RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY LLC YA HOUSTON, TEXAS, MAREKANI MWAKA 2006




Waziri Marmo na Mkuu Lowassa. Picha Mwanakombo


wa Maelezo.

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 119 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007, naomba kutoa taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa tarehe 13 Novemba, 2007 na Bunge hili Tukufu kuchunguza mchakato wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura uliofanyika mapema mwaka 2006 na kuipa ushindi Richmond Development Company LLC ya Houston, Texas, Marekani.



Mheshimiwa Spika, awali ya yote naomba kuchukua fursa hii kwa niaba ya wajumbe wenzangu wa Kamati Teule kukupongeza wewe binafsi na Bunge lako Tukufu kwa uamuzi wa kuunda kamati hii maalum kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya kikatiba ya Bunge katika kuisimamia na kuishauri Serikali na vyombo vyake kwa niaba ya wananchi.

Mheshimiwa Spika, baada ya hoja ya kuundwa kwa Kamati Teule kuwasilishwa na kuafikiwa na Bunge, uliwateua Wabunge watano wafuatao kuunda Kamati Teule ya Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 104(3) ya Kanuni za Bunge, Toleo la 2004:(a) Mhe. Dk. Harrison George Mwakyembe, Mb(b) Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya, Mb(c) Mhe. Mohamed Habib Juma Mnyaa, Mb(d) Mhe. Lucas Lumambo Selelii, Mb(e) Mhe. Herbert James Mntangi, Mb

Soma taarifa ya KAMATI TEULE YA BUNGE ili upate taarifa zaidi.

No comments: