SHIRIKA la ndege nchini (ATC) limeingiza nchini ndege moja kati ya mbili ilizonunua Canada kwa jumla ya dola milioni 16.2. ya kwanza iliyowasili jana ni aina ya Bombadier Dash 8 Q300 yenye kubeba abiria 50. Jumapili itawasili Bombadier Dash 8 Q400 yenye kubeba abiria 74.
Kwa mujibu wa bosi wa ATC, Daudi Mattaka ambaye alianza kushika nafasi hiyo mwezi February mwaka jana, ndege hizo zitaanza na safari za ndani kwenda Kigoma, Tabora, Shinyanga, Zanzibar na Dar na baadaye zitaenda Dodoma, Songea na Sumbawanga.
Mattaka alisema lengo la shirika ni kuwa na ndege 9 zake lenyewe ifikapo mwaka 2012, ikiwa ndege tano kubwa kwa safari za masafa marefu na nne ndogo za masafa ya kati. Hivi sasa shirika lina Boeing 737-200 mbili za kukodi, na inatarajia kukodi zingine mbili mwezi ujao kwa safari za Dubai kupitia Muscat na Afrika Kusini, pamoja na China. Picha ya mdau Muhidin Issa Michuzi.
Comments