Tuesday, February 26, 2008

Wakuu wa vyuo wachimba mkwara

WAKUU wa Vyuo Vikuu vya Umma nchini wamelaani vurugu zilizofanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na kuazimia kuwa watakaobainika wafukuzwe, wasiruhusiwa kusoma kwenye chuo chote nchini wala kupewa mkopo na serikali.

Sambamba na hilo, wakuu hao wametaka wanafunzi wote watakaopatikana na hatia ya kuhusika na vurugu hizo wasimamishwe kuendelea na chuo na kutoruhusiwa kuendelea na masomo katika chuo chochote cha umma nchini, pamoja na kutolewa katika mpango wa serikali wa kuwakopesha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

Vurugu hizo zilizofanyika Ijumaa usiku pamoja na mambo mengine wanafunzi hao sehemu ya Mlimani, walivamia nyumba ya Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, na kuvunja geti wakishinikiza wapatiwe maji.


No comments:

RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE LA NCHI ZA MAZIWA MAKUU (FP-ICGLR) IKULU NDOGO TUNGUU, ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kiongozi wa Jukwaa la Mabunge la...