Friday, February 08, 2008

Mizengo Kayanza Peter Pinda athibitishwa Wazir Mkuu

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Mizengo Kayanza Peter Pinda kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kuchukua nafasi ya Edward Lowassa aliyejizulu jana.

Mizengo Pinda anakuwa Waziri Mkuu wa 10 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitanguliwa na JK Nyerere, Rashid Kawawa, Cleopa Msuya, Edward Sokoine, Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba, John Malecela, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa.

Akitangaza matokeo sasa hivi Spika wa Bunge Samwel Sitta, Pinda amepitishwa rasmi na wabunge kuwa Waziri Mkuu mpya kwa kura 279 za ndio ama asilimia 98.9 wakati kura mbili za hapana na moja imeharibika.

Kuanzia dakika hii mheshimiwa Mizengo Peter Pinda ndiye Waziri Mkuu wetu. Saa tano kamili kesho ataapishwa Ikulu ya Chamwino.

No comments:

Kiwanda cha Tansalt Tanga, Mwarobaini wa Soko la Madini ya Chumvi Nchini

  ☑️ Kiwanda kina uwezo wa kuzalisha tani 5 hadi 8 kwa saa. 📍 Tanga Kiwanda cha Tansalt kilichopo mkoani Tanga kimekuwa msaada mkubwa kwa w...