Thursday, February 07, 2008

Karamagi, Msabaha, Lowassa wajiuzulu




Mpaka muda huu tunaingia hewani ayari mawaziri watatu wameshatangaza nia za kujiuzulu nyadhifa zao kutkana na kashfa mbalimbali wanazokabiliwa nazo ndani ya serikali kwa kuipendelea kampuni ya mkobani na ya kitapeli kama inavyotajwa na ripoti ya kamati ya Dk Harrison Mwakyembe.

Tayari Waziri Mkuu Lowasa alitangaza nia ya kujiuzulu asubuhi, kisha akafuatiwa na Nazir Karamagi, Waziri wa Nishati na Madini ambaye katika uchangiaji wa hoja yake alionekana kuzungumza madudu matupu na kwa kiasi kikubwa aliunga mkono ripoti ya Mwakyembe.


Baadaye alijifananisha na Yesu kwa kujifanya eti hakuwa na dhambi na kwamba anawajibika ili kusudi Watanzania wasife kwa dhambi. Inachekesha.

Aliutumia muda wake mwingi kuzungumzia mambo ya vichekesho huku mara kadhaa akirusha mpira kwa mwenzake Dk Msabaha. Naye Msabaha baada ya kupewa nafasi alitumia muda wake mwngi kufanya mzaha wa matani ya Wazaramo na Wanyamwezi, lakini hakutoa hoja ya msingi ili mradi tu alisimama kutamka nia yake ya kujiuzulu. Picha na Edwin Mujwahuzi.

No comments: