Wednesday, October 08, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AZUNGUMZA NA WANA ISIMANI

10Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika, Oktoba 7, 2014, katika Kijiji cha  Magozi, Kata ya  Ilolo Mpya, akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo la Isimani la Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu na Bunge, William Lukuvi katika wilaya ya Iringa Vijijini, mkoani Iringa. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ISIMANI-IRINGA)1Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Lukuvi wakishiriki kufyatua matofali ujenzi wa Zahanati Kijiji cha Magozi Ilolo Mpya2Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya akiwa katika ziara ya kikagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo la Isimani, wilaya ya Iringa Vijijini. Kushoto ni Mbunge wa jimbo hilo, William Lukuvi3Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsisitizia jambo Lukuvi baada ya kukagua ujenzi wa zahanati hiyo kutoka kshoto ni Hassan Mtenga Katibu wa CCM mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu4Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya sekondari William Lukuvi  Ilolo Mpya.5Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo6Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akieleza sera za Chama wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuzungumza na wananchi kwenye mkutano huo7Mjumbe wa shina namba sita, Changula Mlula akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye kikao cha shina hilo, Kijiji cha  Magozi, Ilolo  Mpya jimbo la Isimani. Kulia ni Mbunge wa Isimani William Lukuvi9Wananchi wa Jamii ya Kimasai wakicheza ngoma kumpokea Kinana wakati wa mkutano huo11Mbunge wa Isimani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu na Bunge, William Lukuvi akieleza alivyotekeleza ilani ya CCM wakati wa mkutano huo12Mbunge wa Isimani William Lukuvi akiwa amemkabidhi kompyuta Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Pawaga Bw. Yusuph Luvanga13Wananchi wa Jamii ya Wasukuma wakicheza ngoma kumlaki Kinana kwenye mkutano huo14Lukuvi akiselebuka na wananchi katika kucheza ngoma wakati wa mapokezi ya Kinana kwenye mkutano huo15Msanii Nyamidela akitumbuiza na wimbo wake maalum unaomzungumzia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpongeza msanii Nyamidela mara baada ya kutumbuiza18Mbunge wa Isimani William Lukuvi akiwa amemkabidhi kompyuta Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya William Lukuvi, iliyopo Kata ya Ilolo Mpya,  Charles Mgimwa (kulia ) wakati wa mkutano huo. Mbali na kuwakabidhi kompyuta walimu wa shule mbili za sekondari aliwataka wananchi kuwa tayari kuunganishiwa umeme wa bei nafuu ambao alisema utaaingia kwenye kata hiyo hivi karibuni.19Mmoja wa wananchi akiuliza swali

No comments:

SAMSUNG IMEFUNGUA MADUKA MAWILI MAPYA YA BRAND STORE KUNDUCHI NA UBUNGO

  Dar es Salaam, Tanzania, 10 Februari 2025: Samsung Electronics East Africa imezindua rasmi maduka mawili mapya ya chapa ya Samsung katika ...