Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akikumbatiana na Mama yake Mzazi wakati wa Kumuaga.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akimuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (katikati) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kulia) wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Mrembo huyo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe,Jijini Dar es Salaam usiku huu.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko (pili kulia),Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kulia) pamoja na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akitoa shukrani zake wakati wa hafla hiyo ya kumuaga iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mh. Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akitoa nasaha zake kwa Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2013,wakati wa hafla ya Chakula cha jioni ikiwa ni sehemu ya kumuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World).Hafla hiyo imefanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko na kushoto ni Mlezi na shoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akizungumza machache ikiwa ni pamoja na kuwaasa Warembo waliopo kambini hivi sasa kujitahidi kufanya vyema.
Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe,Dkt. Charles Bekoni akitoa salamu.
Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza.
Sehemu ya Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa kwenye hafla hiyo.Picha zote na Othman Michuzi
Comments