Mhasibu aibuka mshindi wa Nyumba kupitia Promosheni ya Airtel Yatosha

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya kusaka mshindi wa nyumba wa kwanza kupitia Promosheni ya Airtel Yatosha. Kushoto ni Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Milao, kulia ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga wa kwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha ilimpata mshindi wa Nyumba Bw Silvanus Juma kutoka mkoa wa Iringa.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando, Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Milao (kushoto) na Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga wa kwanza kulia wakisubiri draw ya kutafuta mshindi itafute namba ya mshindi wakati wa kutafuta mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kusaka mshindi wa nyumba wa kwanza kupitia Promosheni ya Airtel Yatosha. Droo ya Airtel Yatosha ilimpata mshindi wa Nyumba Bw Silvanus Juma kutoka mkoa wa Iringa.
Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga wa kwanza kulia akizungumza na simu ya mshindi wa nyumba ya kwanza ya Airtel wakati wa kutafuta mshindi wakati wa kuchezesha droo ya kusaka mshindi wa nyumba wa kwanza kupitia Promosheni ya Airtel Yatosha katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando na  Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Milao (kushoto) . Droo ya Airtel Yatosha ilimpata mshindi wa Nyumba Bw Silvanus Juma kutoka mkoa wa Iringa.

                          **************************************88

Airtel Tanzania imetangaza mshindi wa kwanza wa nyumba  kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Shinda nyumba inayoendelea  na kuwazawadia wateja wake kila siku Bwana Silvanus Juma mkazi wa Iringa mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni mhasibu katika shirila la Tanzania Rural women and children development foundation - TARWOC ameibuka mshindi na kuzawadiwa  nyumba kisasa iliyojengwa na shirika na nyumba la taifa NHC iliyopo kigamboni
jijini Dar es Saalam.

Akiongea wakati wa kuchezesha droo hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel bwana Jackson Mmbando alisema" kama tulivyowangazia awali leo ndio ile siku muhimu na maalumu ya kumpata mshindi wetu wa kwanza wa nyumba  na tumeshuhudia bwana Silvanus Juma  akiibuka mshindi kupitia droo ya kwanza tuliyoichezesha hapa.
Sambaba na hilo leo tunao washindi 7 wa wiki  kutoka katika mikoa mbalimbali ambao hawa wataondoka na pesa taslimu shilingi  milioni moja kila moja, washindi hawa ni pamoja na  Peter Ignasho kutoka Muheza Tanga, Edita Rweyabura  kutoka Bukoba, Steven Maguro , Rakesh Ali Mauji, Mwajuma Hassani kutoka Dar es Saalam, Siasa Yahaya Songo kutoka Manyoni Singida and Vero Mispela Kiwango kutoka Bihalamulo.
Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kuendelea kutumia huduma ya Airtel yatosha na kujiunga na vifurushi mbalimbali na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali , kujiunga nirahisi piga  *149*99# kisha nunua kifurushi chacko cha  siku, wiki au mwezi  na kisha kuingizwa moja kwamoja kweny droo ya kuweza kushinda milioni moja kila siku au zawadi kubwa ya Nyumba.
Akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi Bwan Silvanus Juma alisema"Ninayofuraha sana kupata zawadi hii kubwa kutoka Airtel napenda kutoa wito kwa watanzania na wateja wa Airtel waendelee kutumia huduma ya Airtel yatosha na waamini kuwa hakuna upendeleo.
Binafsi sijawahi kushinda Bahati nasibu yoyote na nilikuwa siamini kama hakuna ubaguzi kwenye kushinda, lakini leo nashuhudia kwamba ushindi ni wa uhakika usio na upendeleo wala ubaguzi hivyo wajaribu nao wanaweza kuwa washindi.
Kwa upande wake moja ya wafanyakazi wenzake Bwana Beatus Magoti ambaye ni Mshauri wa fedha na utawala TARWOC alisema"  tumefurahi sana kuona kijana mgodo mwenzetu ambaye ni mchapa kazi ameweza kushinda nyumba kupitia promosheni ya Airtel yatosha.  Hii imetupa hamasa na sisi kushiriki na kueneza habari kwa wengine kushiriki na kushinda kama
laivyoshinda Silvano.
Airtel inaendelea na promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba tatu ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake na kutoa huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel yatosha.  Sambamba na hilo Airtel pia imewawezesha wateja wake nchi nzima  kutuma na kutoa pesa bure bila makato yoyote.

Comments