Skip to main content
TACAIDS yatoa takwimu za UKIMWI, mkoa wa Njombe unaongoza ukifuatiwa na Iringa
TUME ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) imesema mkoa wa Njombe
unaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya Virusi vya UKIMWI kwa
asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1.
Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya nne kwa asilimia tisa ukifuatiwa na
Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi
(5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).
Msemaji wa TACAIDS, Glory Mziray alisema hayo jana Dar es Salaam na wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Mikoa mingine na viwango vyake ni Mara (4.5), Mwanza (4.2),Mtwara
(4.10), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8),
Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4),
Unguja (1.9) na Pemba (0.3).
Alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi
mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya UKIMWI
yamepungua kwa kasi ndogo.
Alisema watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu
Virusi vya ukimwi na UKIMWI wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha
kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.
Kuhusu tohara kwa wanaume endapo inapunguza maambukizi ya UKIMWI alisema
inapunguza kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja kutoa elimu
zaidi juuya uelewa wa ugonjwa huo.
Comments