RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI SHEIN AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake 

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na  Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton, (katikati) aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe wake, (kushoto) Chalsea Clinton,ni Mtoto wa Rais Mstaafu wa Marekani.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mtoto wa Rais Mstaafu wa Marekani Chalsea Clinton,baada ya kufungua mpambano wa Mpira wa Miguu kwa timu za Wachezaji wa Zamani uliofanyika Jana  katika Uwanja wa Amaan.
 Mtoto wa  Rais Mstaafu wa Marekani Chalsea Clinton,akipiga mpira kama ishara ya kufungua mpambano wa Timu za wachezaji wa zamani katika sherehe za Ziara ya Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton,kukagua miradi mbli mbali katika nchi za Afrika iliyo chini ya ufadhili wa Taasisi yake, (CLINTON FOUNDATION) katika uwanja wa Amaan jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Rais wa Mstaafu wa Marekani Bill Clinton, wakipata maelezo kutoka kwa  Bruno Mnnen,wakati walipotembelea katika banda la utoaji wa huduma ya uchunguzi wa Damu ya Maleria pamoja na Vyandarua,(Clinton Health Access Initiative-CHAI) katika ziara yake Clinton kuangalia miradi mbali mbali katika Nchi za Afrika,(wapili kushoto) Mtoto wa  Rais Mstaafu wa Marekani Chalsea Clinton.Picha na Ramadhan Othman,IKULU-Zanzibar

Comments