Posted by
Vempin Media Tanzania
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akionesha picha ya
kijana Leonard Jeremiah Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye
amekamatwa na kete 86 za madawa ya kulevya kwa wanahabari.…
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akionesha picha ya kijana
Leonard Jeremiah Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa
na kete 86 za madawa ya kulevya kwa wanahabari.
Wanahabari wakimsikiliza Dk. Mwakyembe.
JUHUDI za Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe za
kupambana na dawa za kulevya nchini Tanzana zimeanza kuzaa
matunda baada ya jana akiwa katika ukaguzi wa Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa Julius Nyerere kunaswa kijana akijaribu kupita na
dawa za kulevya katika uwanja huo.
Kwa kile kuoneshwa kukerwa na tabia hizo, Dk. Mwakyembe
amempiga picha kijana huyo ambaye ni rasta na pita yake itasambazwa
maeneo tofauti, huku kesi yake ikiendelea ya kupatikana na madawa
hayo ya kulevya.
Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam
, Dk. Mwakyembe alimtaja kijana aliyekamatwa jana kuwa ni Leonard
Jeremiah Monyo (Edwin Jeremiah Monyo) ambaye amekamatwa na kete
86 za madawa ya kulevya aina ya heroin akitaka kusafiri nazo kuelekea
misokoto ya bangi 34 akiwa ameficha kwenye begi lake.
Alisema kijana huyo rasta alinaswa na mtambo wa kukagua mzigo baada
ya wakaguzi kuushuku mzigo wake hivyo kuamuru ukaguliwe ndipo
alipokutwa na madawa hayo haramu akijaribu kusafiri nayo kwa ndege.
Alisema kijana huyo kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi
zaidi kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukutwa na dawa
hizo haramu. Alisema kwa kile kuoneshwa kukerwa na vitendo hivyo na
kuamua kwa dhati kupambana navyo wamempiga picha kijana huyo na picha
zake zitasambazwa maeneo mbalimbali ili aonekane na umma kujua watua
ambao wamekuwa wakilichafua taifa nje na ndani kutokana na biashara hizo
haramu.
Dk. Mwakyembe amesema atahakikisha anafuatilia kesi ya kijana huyo
hadi itakapoishia ili uona hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika
na vitendo hivyo kukomeshwa. Alisema maofisa wakaguzi wa mizigo
wawili (wote wasichana) ambao walimnasa kijana huyo watazawadiwa
na kupandishwa daraja kutokana na kazi nzuri waliyoifanya.
"Jana tu baada ya ukaguzi wenzetu ambao wanaona kama tunafanya mzaha
jana tena wakapitisha mzigo wa madawa ya kulevya kiwanja cha ndege cha
Dar es Salaam, kwa sababu vijana wetu sasa wameamka na hawataki mchezo
wakamkamata kijana huyo...," alisema.
"Picha yake itasambazwa kila sehemu...sidhani kama tunahitaji upelelezi kwa
sababu tumekukamata na dawa za kulevya. Mimi na viongozi wangu kupitisha
dawa za kulevya akikisha kuuhakikisha.
Alisema kijana huyo alikamatwa majira ya saa mbili na nusu usiku akiwa anasafiri
kwenda nchini Italia kwa kutumia ndege ya kampuni ya Swissair. Alisema kwa sasa kila atakayekamatwa na dawa za kulevya picha yake itasambazwa maeneo mbalimbali ya
nchi ili watu hao wajulikane.
Alisema kwa sasa taratibu zinafanywa ili kuhakikisha mizigo ya abiria wanaowasili
kutoka nje ya nchi kuingia Tanzania nao mizigo ikaguliwe ili kuwabaini wanaoingiza
bidhaa hiyo haramu ichini pia. Aliongeza zoezi hilo litafanyika katika viwanja vya
ndege na bandarini kwa kila mizigo inapowasili.
Alisema lengo ni kuhakikisha viwanja vya ndege vinakuwa salama na kuacha
kutumika vibaya na baadhi ya watu, jambo ambalo limeendelea kulichafua taifa.
Alisem kiwanja cha Dar es Salaam ni kizuri na kina vifaa vya usalama vya kutosha
ila mapungufu yaliyopo ni kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanatumia vibaya
madaraka yao.
Dk. Mwakyembe ameahidi kuwataja na kuweka picha zao hadharani watu ambao
wanajihusisha na madawa hayo ya kulevya. Amesema wanatarajia kutaja majina
ya Watanzania ambao hivi karibuni walinaswa na dawa za kulevya nchini Afrika
Kusini katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo. Alisema Watanzania wengine
wamekamatwa Hong Kong wakihusishwa na dawa hizo na wanafuatilia pia picha
na majina yao yatawekwa hadharani muda wowote.
Comments