Mapokezi ya Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Wapya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiwasili mbele ya jengo la PPF huku akipokelewa kwa shangwe na wafanyakazi wa Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akipewa shada la maua na Afisa Habari Mkuu Idara ya Habari, Bi. Mwanakombo Jumaa kama pongezi kwa kupewa cheo cha Katibu Mkuu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel Laizer akilakiwa kwa shangwe na Mkurugenzi rasilimali watu Bw. Titus Mkapa wakati wa hafla ya kupokelewa na kukabidhiwa kiti cha Unaibu Katibu Mkuu leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel Laizer akipewa mashada ya maua baada ya kupokelewa na wafanyakazi wa Wizara ya Habari kama pongezi ya kupewa cheo cha Unaibu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel Laizer akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) aliyesimama katikati Bw.Clement Mshana, kulia kwake ni Kaimu Mhariri Mtendaji Mkuu wa TSN Bw. Gabriel Ndelumaki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ndg. Habari Assah Mwambene.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel Laizer akisalimiana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bi. Joyce Fissoo wakati alipolakiwa na wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiongozana kwa pamoja kuelekea ofisini.
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seth Kamuhanda akitoa hotuba fupi ya kukabidhi cheo kwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani).Picha zote na Benedict Liwenga
Comments