Thursday, August 22, 2013

Rais Jakaya Kikwete Afanya Mabadiliko ya Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu katika Wizara mbalimbali,Soma Majina na Nafasi Zao


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue Ombeni akitangaza uteuzi wa 
makatibu wakuu na manaibu katika wizara mbalimbali jijini Dar es Salaam 
jana. Picha na Venance Nestory 

----
Imeandikwa na Na Magreth  Kinabo  na Eleuteri  Mangi 
 RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi 
za juu za utendaji wa Serikalini kwenye nafasi za Makatibu Wakuu na
 Naibu Makatibu Wakuu katika Wizara mbalimbali, ambapo  wapo 
waliohamishwa, wataopangiwa kazi nyingine na yumo anayestaafu.


Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
 Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


“Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji
 wa kazi za Serikali katika ngazi hizo za juu,” alisema Balozi Sefue.

Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa Makatibu Wakuu
 ni kama ifuatavyo:
  • Dk Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, 
  • awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  • Joyce Mapunjo amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa
  •  Afrika Mashariki, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, 
  • Biashara na Masoko.

  • Jumanne Sagini amekuwa Katibu  Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu - 
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) awali alikuwa 
  • Naibu Katibu  Ofisi wa Waziri Mkuu - TAMISEMI.

  • Dk Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, 
  • awali alikuwa Naibu Katibu Wizara ya


Fedha.
  • Dk Patrick Makungu amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,
  •  Sayansi na Teknolojia, awali alikuwa  Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.

  • Alphayo Kitanda amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na
  •  Maendeleo ya Makazi, awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu
  •  – TAMISEMI.

  • Dk Shaaban Mwinjaka amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, awali
  •  alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na Masoko.

  • Dk Uledi Mussa amekuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na 
  • Masoko, awali alikuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

  • Profesa Sifuni Mchome amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya  Elimu na 
  • Mafunzo ya Ufundi, awali alikuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo
  •  Vikuu Tanzania.

  • Charles Pallangyo amekuwa Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, 
  • awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri.

  • Anna Maembe amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii 
  • Jinsia na Watoto, awali  alikuwa Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo.

  • Sihaba Nkinga amekuwa Katibu  Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, 
  • Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo.

  • Sophia Kaduma amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na 
  • Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.



Balozi Sefue aliongeza kwamba:

  • Katibu Mkuu aliyepewa uhamisho ni  Peniel  Lyimo ambaye anahamia 
  • Ofisi ya Rais - Ikulu  kwenye “Presidential’s Delivery Bureau” kama Naibu 
  • Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi
  •  ya Kilimo mwanzoni alikuwa  Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu.



Makatibu wakuu watakaopangiwa kazi nyingine ni:-

  • Sethi Kamuhanda aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, 
  • Utamaduni na Michezo 
  • Kijakazi Mtengwa aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii
  •  Jinsia na Watoto 
  • Injinia Omari  Chambo aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi



Katibu anayestaafu ni Patrick Rutabanzibwa ambaye alikuwa Katibu 
Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye sasa 
amestaafu kwa hiari.


Aidha, Balozi Sefue alisema Rais Kikwete pia amefanya uteuzi wa Naibu
Makatibu Wakuu wapya na kuwapa uhamisho baadhi yao.  Aliiwataja
Naibu Makatibu Wakuu wapya walioteuliwa kuwa ni:-

  • Angelina  Madete amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa 
  • Rais  Mazingira

  • Regina Kikuli amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu

  • Zuberi Sumataba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu 
  • – TAMISEMI, anayeshughulikia  suala la elimu katika ngazi za Serikali
  •  za Mitaa

  • Edwin Kiliba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu 
  • - TAMISEMI

  • Deodatus Mtasiwa amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
  •  - TAMISEMI ambaye atashughulikia saula la afya  upande wa  Serikali za Mitaa.

  • Dk Yamungu Kayandabila amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara
  •  ya Kilimo, Chakula na Ushirika

  • Profesa Adolf Mkenda amekuwa Naibu Katibu Mkuu ya Fedha 
  • anayeshughulikia sera

  • Dorothy Mwanyika amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Fedha 
  • anayeshughulikia Fedha za Nje na Madeni

  • Rose Shelukindo amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na 
  • Jeshi la Kujenga Taifa

  • Dk Selassie Mayunga amekuwa Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya Ardhi, 
  • Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  • Monica Mwamunyange amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi

  • Consolata Mgimba amekuwa  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Elimu na 
  • Mafunzo ya Ufundi

  • Profesa Elisante ole Gabriel Laizer amekuwa Naibu Katibu Mkuu 
  • Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

  • Armantius Msole amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano
  •  wa Afrika Mashariki



Balozi Sefue aliwataja Naibu Makatibu Wakuu waliopewa 
uhamisho kuwa ni:-

  • John Mngondo ambaye amehamishiwa Wizara ya Wizara ya Mawasiliano
  • , Sayansi na Teknolojia ametoka Wizara ya Uchukuzi katika nafasi hiyo

  • Selestine Gesimba amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, anatoka
  •  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

  • Injinia Ngosi Mwihava anahamia Wizara ya Nishati na Madini kutokea
  •  Ofisi ya Makamu wa Rais

  • Maria Bilia amehamia Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka Wizara ya 
  • Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 

  • Nuru Milao anahamia  Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto 
  • kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

No comments: