MAKUMBUSHO WAFUZU MAFUNZO YA ULINZI SHIRIKISHI

  Mhitimu wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni ,Ally Vumbi(kushoto)akipiga saluti kwa Mkuu wa Wilaya, Jordan Rugimbana mara baada ya kutunukiwa cheti baada ya kumaliza mafunzo ya ulinzi shirikishi Dar es Salaam jana.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana(kulia) akimkabidhi cheti, Mtendaji wa Kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni , Husna Nando wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi  Dar es Salaam jana.
 Mkuu wa mafunzo ya Ulinzi Shirikishi Kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni, Koplo Ibrahim Omari akitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya Jordan Rugimbana kwa kupisha zoezi la kutoa mafunzo ya ulinzi shirikishi kuwa la Wilaya nzima wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi Dar es Salam jana.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani Mkuu wa mafunzo ya Ulinzi Shirikishi Kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni, Koplo Ibrahim Omari wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Polisi jamii wa Barabara ya Kilwa,wakiwa kwenye gwaride na mbwa waliopewa mafunzo maalumu ya ulinzi shirikishi wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ulinzi shirikishi wa Kata ya Makumbusho Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana(kushoto) akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi na wakati wa Kata ya Maakumbusho wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu hao Mwananyamala jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Machellah.
  ------
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni,Jordan Rugimbana ametoa muda wa miezi mitatu,Kata zote za Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ziwe zimeshaanzisha vikundi vya Ulinzi shirikishi na kiongozi yeyote atakaekaidi agizo hilo basi anashiriana na wahalifu.
Rugimbana aliyasema haya wakati wa hafla ya kukabidhi Vyeti kwa wahitimu wa 40 waliofuzu mafunzo ya ulinzi shirikishi kata ya Makumbusho Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo pia ametoa fursa ya baadhi ya wahitimu kwenda Polisi Kilwa Road kupata elimu ya kutumia Mbwa katika kazi ya ulinzi shirikishi baada ya kuvutiwa na vijana wa Polisi jamii walioonyesha gwaride pamoja na mbwa katika hafla hiyo.
Alisema Rugimbana,”Nendeni mkafanye kazi na mtakapo pata kikwazo niambieni niko tayari kudili na mtu wa yeyote,kafanyeni kazi kwa ufasaha muipe sifa Kata ya Makumbusho na Wilaya nzima ya Kinondoni kwa kumaliza kabisha swala la uhalifu,madawa ya kulevya  pamoja na usafi wa mazingira”.
Rugimbana alisema kuanzia sasa mtu yeyete atakayekamatwa kwa uchafuzi wa mazingira faini ni fedha taslimu shilingi 50,000/= na hiyo pesa ni ya kwako wewe uliyemkamata.
 Aidha Mkuu wa Wilaya alichangia mfuko wa Polisi jamii Kata ya Makumbusho kiasi cha Shilingi 1,000,000/= pamoja na kuwa mlezi wa Polisi jamii wa Wilaya nzima.
Akitoa shukrani kwa Mkuu wa Wilaya,Diwani wa Kata ya Makumbusho, Ally Haroub aliwaomba wakazi wa makumbusho kutoa ushirikiano katika swala la ulinzi shirikishi ili kupunguza uhalifu, madawa ya kulevya na swala la mazingira kwa kutoa tofauti zao za kidini,kabila wala umri kwani kipindupindu hakichagui dini ,kabila wa la Kiongozi.
Mafunzo ya wahitimu ya vijana wa ulinzi shirikishi yametumia muda wa miezi miwili chini ya Koplo Ibrahim Omary kutoka kituo cha Polisi Ostarbay yenye madhumuni ya kuunganisha polisi na jamii ili kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano katika kuondoa kero za uhalifu,kutatua matatizo ya uhalifu na kuondoa hofu ya usalama wa jamii husika.
Wakisoma risala wahitimu hao kuwa mafunzo waliyopata ni huduma bora kwa wateja,ukakamavu,dhana ya polisi jamii,nidhamu,ukamataji salama wa mhalifu,uwasilishaji taarifa,sheria ndogo nogo za ulinzi,usafi na mazingira na pia walipata nafasi ya kutembelea kikosi cha mbwa na farasi.
Mwisho walizindua mfuko wa Ulinzi shirikishi ambao kila mwananchi atakayeguswa na huduma yao achangie ambayo ni 03201000035 Dar es Salaam Commuty Bank Tawi la Magomeni.

Comments