Thursday, August 15, 2013

Polisi wamkamata aliyemuua Msuya

Polisi wamefanikiwa kumtia mbaroni mfanyabiashara tajiri wa madini ya Tanzanite huko Mirerani anayetajwa kuwa ndiye aliyepanga na kukodi watu waliomuua bilionea Erasto Msuya.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zimedai kuwa mfanyabiashara huyo alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana na juzi alikuwa akihojiwa na makachero.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mfanyabiashara huyo ndiye aliyetoa fedha za kununulia pikipiki mbili zilizotumika katika mpango huo na pia alitoa fedha kwa ajili ya kununua simu mpya na laini mpya.
“Tumewakamata watu wametupa mwanga mzuri na huyo mfanyabiashara ndiye aliyetoa fedha za kununua pikipiki na siku moja kabla ya tukio zilihifadhiwa nyumbani kwake,” alidokeza polisi mmoja.
Habari hizo zimedai kuwa polisi pia imewahoji mawakala wa kampuni za simu ambao walitumiwa kusajili laini mpya za simu zilizotumika kumpigia marehemu na kutumika kupanga mauaji hayo.
Pikipiki hizo mbili, zilinunuliwa siku moja kabla ya tukio zikahifadhiwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo hadi siku iliyofuata ambapo aliwakabidhi wauaji na zote zimekamatwa.
Mahojiano kati ya mfanyabiashara huyo na Polisi yamekuwa yakifanyika kwa siri na katika kituo cha polisi (jina tunalo) na kwamba mambo ni mazuri.
lakini hakitatajwa jina lake.
SOURCE:MWANANCHI

No comments: