Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa, Kuwasili Mkoani Tanga Kuzindua Mabaraza ya Katiba ya Chadema Pamoja na Kuhutubia Mikutano ya Hadhara
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa
---
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, Alhamisi wiki hii anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga kuzindua mabaraza ya Katiba ya chama hicho pamoja na kuhutubia mikutano ya hadhara.
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje, ilieleza alisema Dk. Slaa atawasili mkoani hapa Agosti 15 na kufanya mikutano ya hadhara na siku inayofuata atakuwa na kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari, Bahweje alisema Dk. Slaa akitumia helikopta atafanya mikutano ya hadhara katika wilaya za Lushoto, Handeni, Korogwe, Muheza na Tanga Jiji.
“Katibu mkuu atawasili Lushoto na kufanya mkutano wa hadhara uwanja wa RRM saa mbili asubuhi, Handeni mjini saa 5.30 asubuhi, Korogwe Mazoezi saa 7.30 nchana, Muheza saa 9.30 uwanja wa CHADEMA Square na mkutano wa mwisho Tanga Jiji saa 11. 40 jioni,” alisema Bahweje.
Katibu huyo alitoa wito kwa wananchi kuhudhuria mikutano hiyo katika maeneo hayo na kumsikiliza ili kupata misingi halisi ya mikutano hiyo.
Sambamba na hayo, alieleza chama hicho ngazi ya mkoa kinaendelea na mikutano ya hadhara na ya ndani kwa kuanzia wilaya ya Korogwe kwa lengo la kuelezea mkakati wa CHADEMA.
Alisema mikutano hiyo inafanyika katika vijiji vya Masange, Mngwasa na Lutindi vya kata ya Lutindi na kuendelea katika kata ya Bungu, jimbo la Korogwe vijijini.
Comments