JK apata futari na kina Shilole

NI msimu wa futari ambao unaelekea ukingoni mwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani! Baadhi ya mastaa wa Bongo Fleva na filamu wamepata mwaliko wa futari kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alijiachia nao ikulu.
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msanii Zuwena Mohamed a.k.a. Shilole.
Walianza wasanii wa Bongo Fleva na baadhi ya watangazaji wa Bongo ambao mwishoni mwa wiki iliyopita walikusanyika kwenye futari hiyo ikulu iliyopo maeneo ya Magogoni, Dar.
Wakiwa ikulu, mastaa hao waligonga mnuso wa maana pamoja na kwamba siyo wote walioalikwa walikuwa wamefunga.
Baadaye JK aliwapa neno la kuwatia moyo kuendelea kufanya muziki mzuri utakaopendwa na watu wote na wa kimataifa.
JK aliwahakikishia kuwa huwa anasikiliza muziki wao hivyo waongeze bidii.
Rais Kikwete akimpa tano Msanii Mkongwe wa Bongofleva, Gwamaka Kaihula a.k.a King Crazy G K.
JK AGONGA TANO!
Pia JK, sambamba na First Lady, Salma Kikwete walionekana wachangamfu huku prezidenti ‘akipewa tano’ kama sehemu ya swaga kutoka kwa baadhi ya wasanii kama Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’.
Kidogo tu kadosari kalitaka kujitokeza kwa vazi alilotinga Shilole kwani lilikuwa ‘transiparenti’ kiasi cha kuonesha rangi ya sidiria na ‘vifuu’ vyake kifuani.
Baadhi ya mastaa walioalikwa ni pamoja na prodyuza P- Funk, Lamar, AY, TID Mnyama, Marlaw, Chegge, Hemedy, Shilole, Mwasiti, Ali Kiba, Jafarai, Aslay, Fella, Ferouz, Z-Anto, Madee, Keisha, Nay wa Mitego, Linex na wengine wengi huku wale wa filamu wakialikwa kwenye futari Jumamosi iliyopita.

MASTAA WALIOFUTURU KWA SNURA WANAHITAJI BAKORA
Wakati huohuo, Ijumaa iliyopita staa wa muziki na filamu za Kibongo, Snura Mushi naye alifuturisha nyumbani kwake lakini kukawa na dosari moja kubwa.
Katika futari hiyo iliyoendana na kumpongeza mtoto wa Snura kwa kufikisha miaka 3, iliyofanyika nyumbani kwake Mwananyamala, Dar, baadhi ya mastaa waliohudhuria wanahitaji kutandikwa bakora kwa kitendo walichokifanya.
Baadhi ya mastaa hao walikula futari na dakika chache baadaye walihamia baa iliyopo jirani na nyumbani kwa staa huyo kisha wakaanza kutandika bia ili kushushia futari, jambo ambalo ni kinyume na taratibu za mfungo.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa suala hilo ni sawa na kukejeli au kumkufuru Mwenyezi Mungu kwani inajulikana kuwa futari ni chakula kinacholiwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani lakini kwa upande wa mwigizaji na msanii wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda na wenzake waliokaa baa waliona ni kitendo cha kawaida.
“Unajua hawa mastaa wanakufuru sana, nini maana ya kufuturu ‘theni’ unahamia baa kunywa pombe? Hiki ni kitendo kibaya sana wamemdhalilisha mwenzao aliyewaalika, unadhani atajisikiaje akipewa taarifa kuwa wapo nje wanakunywa?
“Wameona baa wameshindwa kuvumilia, hii ni tabia mbaya mno,” alisema msanii mmoja ambaye hakutaka jina lipambe ukurasa huu.
Mbali na Isabela, wengine walionaswa baa dakika chache baada ya kufuturu kwa Snura ni pamoja na Jacqueline Pentzel na shosti wake (Mariam), msanii mmoja wa komedi na chipukizi wa filamu.
Mbali na kukaa baa, Jack na Mariam  walikuwa wakirushiana vijembe mbele ya watu kitendo ambacho kilionesha wazi kuwa si sahihi kwa watu kugombana eneo la kufuturu kulingana na mwezi kwani unahitaji stara.

Comments