TAMASHA LA IDD MOSI DAR LIVE: WASANII, MABONDIA WALONGA NA WANAHABARI

Meneja wa Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili kulia) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu burudani mbalimbali zitakazokuwepo Dar Live sikukuu ya Idd Mosi. 
 
Mwanamuziki H - Baba akitamba mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuwa atafunika mbovu siku hiyo.
Mratibu wa mapambano ya ndondi, Abdallah Yasin 'Ustaadh' (kulia) akiongea na wanahabari. Kushoto niAbdallah Mrisho.
Mwanamuziki Ali Kiba (kulia) akipeana 'hi' na Ustaadh wakati wa mkutano huo.
 
Bondia Francis Miyeyusho akitunisha misuli. Bondia huyu atapigana na Mzambia Darius Lupupa.
 
Bondia Chupaki Chipindi atakayezipiga na Ramadhan Kido.
 
 Ramadhan Kido atakayepambana na Chupaki Chipindi siku hiyo.
 
Mabondia wa kike Ester Kimbe (kushoto) na Irene Kimaro wakijaribu kuzipiga.
Mabondia Francis Miyeyusho (kulia) na Ramadhan Kido (kushoto) wakifuatilia mkutano huo.
 
Chupaki Chipindi kutoka mkoani Iringa akiwa kwenye pozi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
 
Bondia Ester katika pozi.
 
 Bondia Irene naye akiwa kwenye picha ya pozi.
 
H - Baba katika pozi la kusimama.
 
Ester ndani ya gloves.
---
WASANII wa muziki watakaopanda katika jukwaa la kisasa la Dar Live sikukuu ya Idd Mosi pamoja na mabondia leo wamelonga na wanahabari kwenye mkutano uliowakutanisha ambao umefanyika katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo wasanii wametambiana kila mmoja akitamba kuwa atamfunika mwenzake. Vilevile mabondia nao wametunishiana misuli hali inayoonyesha kuwa kutakuwa na bonge la burudani katika sikukuu hiyo ya Idd Mosi.

Katika sikukuu hiyo wasanii Ali Kiba, H-Baba, Chegge, Temba, Dogo Aslay, Bi. Cheka na Bendi ya Mapacha Watatu watashusha bonge la burudani na kuwapa raha mashabiki watakaohudhuria shoo hiyo. Kwa Upande wa masumbwi bondia Francis Miyeyusho atazipiga na Darius Lupupa kutoka nchini Zambia, Chupaki Chipindi atapigana na Ramadhan Kido. Vilevile mabondia wa kike Ester Kimbe na Irene Kimaro wataonyeshana moto siku hiyo.PICHA: SHAKOOR JONGO /GPL

Comments