Posted by
Vempin Media Tanzania
on
- Get link
- X
- Other Apps
Msajili wa Vyama vya Siasa mpya, Jaji Francis S.K.Mutungi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K.Mutungi kuwa Msajili
wa Vyama vya Siasa.
Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa
saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi
huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.
Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa
Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma
kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Kanda ya Dodoma.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Comments