Tuesday, August 06, 2013

Vodacom Yafuturisha Pemba

 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akizungumzia kampeni ya Pamoja na Vodacom namna inavyotekelezwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kuandaa futari na kutoa sadaka ya vyakula na vifaa vya shule kwa wanafunzi wa madrasa sehemu mbalimbali nchini. Mwaka huu Vodacom Foundation ilitenga Sh. 50 Milioni kwa ajili ya kampeni hiyo na kuwafikia wanafunzi zaidi ya 2500.
 Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Jaffary Juma akikabidhi vyakula vilivyotolewa na Vodacom Foundation kwa wanafunzi wa madrasa mbalimbali za Kisiwani Pemba tukio lililohusisha pia futari kwa ajili ya wanafunzi hao na wadau wa Vodacom Kisiwani humo iliyofanyika uwanja wa Gombani mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis(mwenye koti jeusi) na Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh (kulia) na wafanyakazi wa Vodacom.
 Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis(mwenye koti jeusi) na Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom na baadhi ya wanafunzi wa Madrasa za Kisiwani Pemba mara baada ya zoezi la kukabidhi sadaka ya vyakula na vifaa vya shule kwa wanafunzi hao muda mfupi kabla ya wote kushiriki futrari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwenye uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba mwishoni mwa wiki
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis akisalimiana na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Uwanja wa Gombani Pemba tayari kuongoza hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na Vodacom Foundation mwishoni mwa wiki kwa ajili ya wanafunzi wa Madrasa na wadau wa kampuni hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh

No comments: