Thursday, August 15, 2013

Rais Jakaya Kikwete amteua Adam Mayingu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)


 Adam Mayingu
--
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Adam H. Mayingu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam, Jumanne, Agosti 13, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi unaanzia Juni 8, mwaka huu, 2013. 
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mayingu alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa PSPF.Bwana Mayingu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria. 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
14 Agosti, 2013

No comments:

WIZARA YA AFYA YAOMBA SH. TRILIONI 1.8 BAJETI YA 2026/2027

  Wizara ya Afya imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi trilioni 1.8 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma z...