Tuesday, August 20, 2013

NHC yakabidhi kwa wakandarasi miradi mitatu mikubwa ya ujenzi

Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye akibadilishana mawazo na viongozi wa NHC.
Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye akibadilishana mawazo na viongozi wa NHC.
 Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye akizungumza katika hafla hiyo Serena leo mchana.
Mkurugenzi Mkuu a Shirika la Nyumba la Taifa , Nehemia Kyando Mchechu (kushoto) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye baada ya makabidhiano kwa mkandarasi wa ujenzi wa Wakulima Village, EstimConstruction Company Limited.
 Mkurugenzi Mkuu a Shirika la Nyumba la Taifa , Nehemia Kyando Mchechu (kushoto) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye baada ya makabidhiano kwa mkandarasi wa ujenzi wa Golden Anniversary Towers. China Railways Jianchan Engineering Company Ltd.
 Mkurugenzi Mkuu a Shirika la Nyumba la Taifa , Nehemia Kyando Mchechu akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Adhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye baada ya makabidhiano kwa mkandarasi wa ujenzi wa Ushindi Group Six Internatonal Ltd.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelezo mafupi ya miradi hiyo.
 Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Issack Peter akitoa maelezo mafupi ya miradi hiyo.
 Mchoro wa namna litakavyokuwa jengo la Wakulima Village litakaloanza kujengwa katika kitalu namba 67 kwenye makutano ya mitaa ya Ngano na Wakulima, Dar es Salaam litakapokamilika litakuwa na ghorofa 16 na kuwa makazi ya watu zaidi ya 840 wakati kabla lilikuwa makazi ya familia moja.
 Mchoro wa namna litakavyokuwa jengo la Golden Anniversary Towers  litakaloanza kujengwa katika kitalu namba 1088 katika makutano ya mitaa ya Magore na Vijibweni, Ilala, Dar es Salaam litakapokamilika litakuwa na ghorofa 26 na kuwa makazi ya watu zaidi ya 1,200 wakati kabla lilikuwa ofisi iliyokuwa na watu chini ya 150.
 Mchoro wa namna litakavyokuwa jengo la Ushindi Residential Apartments litakaloanza kujengwa katika kitalu namba 36 na 37 barabara ya New Bagamoyo, Kinondoni, Dar es Salaam litakapokamilika litakuwa na ghorofa 16 na kuwa makazi ya watu zaidi ya 720 wakati kabla lilikuwa makazi ya familia zisizozidi 10.
 Eneo la mradi la Upanga yatakapojengwa majengo mawili pacha ya ghorofa 26 kila moja yatakayogharimu zaidi ya Shilingi bilioni 68. Eneo lipo katika makutano ya barabara ya Magore na Vijibweni.
 Eneo la mradi la Upanga yatakapojengwa majengo mawili pacha ya ghorofa 26 kila moja yatakayogharimu zaidi ya Shilingi bilioni 68.
Eneo la mradi la Hananasif yatakapojengwa maghorofa mawili yenye ghorofa 16 kila moja yatakayogharimu zaidi ya Shilingi bilioni 24.
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
MAELEZO MAFUPI YA MIRADI YA NHC INAYOKABIDHIWA KWA WAKANDARASI LEO AGOSTI 20,2013
1. Mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi wa Golden Anniversary Towers
Upo kwenye Kitalu nambari 1088 kwenye makutano ya mitaa ya Magore na Vijibweni, Upanga, Manispaa ya Ilala Dar es Salaam. Ni mkabala na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na jengo refu la Uhuru Peak. Ni takriban mita 200 kutoka Posta mpya na mita 250 kutoka  katika ofisi mbalimbali za Wizara za Serikali.
Jina la mradi huu limetokana na Shirika la Nyumba la Taifa kutimiza miaka 50 tangu lianzishwe mwaka 1962.
Kiwanja kina eneo la mita za mraba 4704.9.
Utahusisha ujenzi wa majengo mawili pacha ya ghorofa 26 kila moja yatakayogharimu shilingi 68,337,339,540.60.
Mradi unatarajiwa kuwa na sehemu za makazi 200, ambapo 24 zitakuwa nyumba za chumba kimoja kilichojitosheleza kwa kila kitu, 56 zitakuwa za vyumba viwili na 112 zitakuwa za vyumba vitatu na nyumba kubwa 8. Pia kutakuwa na maegesho ya kutosha yanayotosha wakazi wote.
Nyumba za vyumba viwili zitakuwa na ukubwa wa mita za mraba 80 (sq.m)na zile za vyumba vitatu zitakuwa na ukubwa wa mita za mraba 120. Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo la watoto kuchezea, eneo maalum la kukusanyia taka, maegesho ya magari ya ziada, sehemu ya kuhifadhia maji, eneo la kufanyia mazoezi, bwawa la kuogelea na jenereta.
Mradi unatarajia kutoa ajira za moja kwa moja 1,800 na kuwahifadhi zaidi ya watu 1,200.
Mkandarasi msimamizi wa mradi huu ni China Railways Jianchan Engineering Company Limited.
2. Mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi wa Ushindi
Upo kwenye vitalu nambari 36 na 37 sambamba na barabara ya New Bagamoyo Road, eneo la  Kijitonyama, Manispaa ya Kinondoni- Dar es Salaam.
Mradi umepakana na kituo cha mafuta cha Victoria.
Kiwanja kina eneo la mita za mraba 8091.7
Utahusisha ujenzi wa majengo matatu ya ghorofa 16 kila moja yatakayogharimu shilingi 30,278,718.998.68.
Mradi unatarajiwa kuwa na sehemu za makazi 190, ambapo 112 zitakuwa za vyumba vitatu na 72 zitakuwa za vyumba viwili na nyumba kubwa 6. Nyumba za vyumba viwili zitakuwa na ukubwa wa mita za mraba 80 (sq.m)na zile za vyumba vitatu zitakuwa na ukubwa wa mita za mraba 100. Ujenzi unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24.
Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo la watoto kuchezea, eneo maalum la kukusanyia taka, maegesho ya magari ya ziada, sehemu ya kuhifadhia maji, eneo la kufanyia mazoezi na jenereta. Pia kutakuwa na maduka, mgahawa, super market.
Mradi unatarajia kutoa ajira za moja kwa moja 690 na kuwahifadhi zaidi ya watu 720.
Mkandarasi msimamizi wa mradi huu ni kampuni ya Group Six International Limited.
3. Mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi wa Wakulima
Upo kwenye kitalu nambari 67 kwenye makutano ya mitaa ya Ngano na Wakulima, eneo la  Hananasif, Manispaa ya Kinondoni- Dar es Salaam.
Mradi upo kilomita mbili kutoka katikati ya mji na unafikika kwa urahisi.
Kiwanja kina eneo la mita za mraba 4056.9
Utahusisha ujenzi wa majengo mawili ya ghorofa 16 kila moja yatakayogharimu shilingi 24,912,373,160.35.
Mradi unatarajia kutoa ajira za moja kwa moja 1,140 na kuwahifadhi zaidi ya watu 840.
Mradi unatarajiwa kuwa na sehemu za makazi 120 za vyumba vitatu za ukubwa wa mita za mraba 120 kila moja. Sifa za ziada za mradi huu ni kuwa na ofisi ya meneja wa mradi, eneo la watoto kuchezea, eneo maalum la kukusanyia taka, maegesho ya magari ya ziada, sehemu ya kuhifadhia maji, eneo la kufanyia mazoezi na jenereta.
Mkandarasi msimamizi wa mradi huu ni kampuni ya Estim Construction Company Limited. Miradi yote hii itasimamiwa na Taasisi ya BICO ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

No comments: