Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wafanikiwa kuwatenganisha pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili

Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Muhimbili, Profesa Karim Manji (wa pili kushoto) akifurahia na wenzake baada ya kufanikiwa kwa operesheni ya kuwatenganisha watoto walioungana, kazi iliyofanywa na jopo la madaktari bingwa saba kwa saa 4. Picha na Michael Jamson
---
  Jopo la Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa ya hospitali hiyo (Moi), wamefanikiwa kuwatenganisha pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili.
 
Iliwalazimu mabingwa hao kutumia saa nne kufanikisha upasuaji huo. Mmoja wa watoto hao waliotenganishwa, amelazwa kwenye Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa Moi wakati kiwiliwili kingine kilifariki.
Jopo la madaktari waliofanikisha upasuaji huo ni; bingwa mstaafu wa watoto ambaye aliitwa maalumu kwa kazi hiyo, Petronila Ngiloi, Dk Robert Mhina (mifupa) na Profesa Karim Manji aliyekuwa akifuatilia kwa karibu mapigo ya moyo.
Wengine ni Dk Karima Khalid aliyekuwa akiratibu dawa ya usingizi, Dk Hamis Shaaban (ubongo na uti wa mgongo), Dk Zaitun Bokhary (bingwa upasuaji watoto) na Dk Nyangasa (moyo na mishipa ya fahamu).Kwa habari zaidi bofya na Endelea......>>>>>

Comments