Wednesday, July 24, 2013

Ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wilayani Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi  la ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia  maji wa Kampuni ya Andoya Hydroelectric Company katika kijiji cha Lifakara wilayani  Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi  wa Kampuni hiyo, Menas Andoya
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa kupeleka   umeme  Mbambabay  katika wilaya mpya ya Nyasa  kutoka kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013. Kulia ni Mkewe Tunu na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabiti Mwambungu. Watatu Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiendesha pikipiki wakati alipozindua  Mradi wa Pikipiki wa Kikundi cha SACCOS ya vijana wa Mbinga kwenye uwanja wa CCM mjini Mbinga  akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapongeza baadhi ya waendesha pikipiki wa Mbinga baada ya kuzindua  mradi wa pikipiki za kikundi cha SACCOS ya vijana wa Mbinga kwenye uwanja wa Mpira wa CCM mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakizungumza na Mzee Andrea Mapunda (84) wakati alipotembelea shamaba la kahawa la mzee huyo katika kijiji cha Masumuni wilayani Mbinga wakiwa katika ziar ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.

No comments: