Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati ambapo waandishi hao walitembelea eneo la kibada wilaya ya Temeke kujionea Nyumba 3 zinazoshindaniwa katika promosheni ya Airtel Yatosha. Nyumba hizi zimenunuliwa na Airtel toka shirika la nyumba la taifa kwaajili ya promosheni ya AIRTEL shinda Nyumba 3.

Afisa Uhusiano wa NHC YAHAYA CHARAHANI amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati ambapo wanahabari toka vyombo mbali mbali walitembelea nyumba hizo kujionea jinsi mradi unavyokwenda “nyumba hizi tatu zenye thaman ya shilingi milioni 194 zimekamilika na pindi washindi watakapotangazwa wataweza kuhamia katika nyumba hizi mara moja tu.
Amesema nyumba hizo ambazo ni za kisasa zitakidhi mahitaji ya wengi kwani ujenzi wake umezingatia mahitaji ya familia kubwa. Nyumba hizi zina vyumba vitatu vya kulala, jiko, sebule nzuri pamoja na sehemu ya nje iliyonakishiwa kwa umakini ili kuipa nyumba mvuto wa hali ya juu. Aliongeza bw, CHARAHANI Pia alibainisha kuwa wateja wa kampuni ya airtel wanaweza kuzitembelea nyumba hizo na kujionea wenyewe kiwango cha ubora wa nyumba hizo.
“Hizi nyumba ziko wilaya ya Temeke eneo la kibada karibu kabisa na Tuangoma ambapo hadi kufika katika nyumba hizi ni umbali wa kilomita 2 tu kutoka kituo cha basi kilipo, eneo ambalo linafikika na linamakazi mzuri sana” alimalizia kwa kusema Bw, CHARAHANI.
Nae Meneja Uhusiano wa Airtel JACKSON MMBANDO amewataka watanzania kuendelea kutumia mtandao wa airtel hususani huduma ya yatosha kwa kupiga *149*99# na kuchagua vifurushi vinavyowatosha ili kujihakikishia nafasi ya kushinda nyumba hizo.
Amesema airtel imedhamilia kutatua matatizo ya wateja wake kwa kutoa huduma nafuu na bora kuliko mtandao wowote lakini pia promosheni hiyo ya YATOSHA inalenga kubadilisha maisha ya watanzania hasa wale wanaotumia mtandao wa airtel Amesema katika promosheni hiyo jumla ya shilling million 284 zitatumika kuwazadia wateja wa kampuni hiyo ambapo milioni 194 zitanunua nymba hizo 3 toka shirika la nyumba na kiasi kinachobaki kwa siku 90 Airtel itatoa milioni moja kwa mshindi mmoja kila siku.
No comments:
Post a Comment