Wednesday, July 31, 2013

Majina ya Wanafunzi Waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Mwaka wa Masomo 2013/2014 Haya Hapa


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dr Shukuru kawambwa. 
---
Serikali imetangaza majina ya wanafunzi 18,754 waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu vilivyo chini yake ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 1,659 ikilinganishwa na 17,095 waliochaguliwa mwaka jana.

Kati ya wanafunzi hao, 11,806 wamechaguliwa kusomea ngazi ya cheti (Grade A) na 6,948 watasoma katika ngazi ya stashahada.Wanafunzi 363 wamechaguliwa kusoma elimu maalumu kwa ngazi ya cheti huku 57 wakisoma elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada.
---

MAELEKEZO MUHIMU:

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu mwaka wa masomo 2013/2014 wanatakiwa kuripoti katika Vyuo walivyopangiwa tarehe 15/08/2013.

Fomu ya maelekezo (joining instruction) itatumwa kwa mhusika kupitia anuani yake. Aidha, fomu hizi zinapatikana pia kwenyetovuti hii  kwa kubofya katika link ya Chuo husika.
Wanafunzi wanatakiwa kufika Vyuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
  1. Vyeti halisi vya Baraza la Mitihani la Tanzania kidato cha NNE na SITA kulingana na kozi husika;
  2. Ada ya muhula wa kwanza sh.100,000/= au ya mwaka sh. 200,000/=;
  3. Sare ya Chuo kulingana na maelekezo ya Chuo husika; na
  4. Fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi.

Mkuu wa Chuo anatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa Chuoni ni wale waliopo kwenye orodha hii tu na SI vinginevyo.

Usajili wa waliochaguliwa kujiunga na Vyuo utafungwa tarehe 25/08/2013 saa 12.00 jioni.

*Bofya namba 1 au 2 hapa chini ili kupakua nakala yenye orodha ya majina


 
  1.  WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI 2013/2014 (1.64 MB)
  2.  WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA 2013/2014 (997.5 kB)

No comments: