Mdau Bakari Machumu Aula,Ateuliwa Kuwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Limited (MCL)

Bakari Machumu  
---
Dar es Salaam. Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), imemteua Bakari Machumu kuwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL.
Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Tido Mhando alisema uteuzi huo ulianza rasmi Julai Mosi, mwaka huu na kwamba ni sehemu ya mabadiliko yanayokusudia kuendeleza kampuni hiyo ya habari inayoongoza nchini.
“Katika kazi yake mpya Machumu ataongoza chumba cha habari, sera na mikakati ya maendeleo katika magazeti na shughuli za elektroniki ili kudumisha taratibu za MCL kama kituo cha ubora wa uandishi wa habari. Ninaomba tuungane kumpongeza katika kazi yake hiyo mpya ambayo ni changamoto kwake katika kuendesha vyombo vyetu vya magazeti na elektroniki,” alisema Mhando.
MCL inachapisha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumamosi, Mwananchi Jumapili, The Citizen, The Citizen on Saturday, The Citizen on Sunday na Mwanaspoti na kwenye mtandao.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea.......>>>>

Comments