Msanii 
wa muziki wa asili Tanzania ambaye pia ni msanii wa maigizo na filamu, 
Mrisho Mpoto akizungumza jambo mbele ya waaandishi wa habari na wamiliki
 wa blogs mbalimbali katika uzinduzi wa matumizi mazuri ya mitandao ya 
kijamii. Mrisho alisimama kuzungumza dakika chache baada ya wimbo 
alioimba na Banana Zoro kuzinduliwa, unaojulikana kama 'Futa, Delete 
Kabisa'. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano 
Tanzania (TCRA),John Nkomo katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi
 Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkomo, 
akizungumza mbele ya wamiliki wa blogs mbalimbali Tanzania, waandishi wa
 habari katika warsha ya kampeni ya kuzindua matumizi mazuri ya mitandao
 ya kijamii kwa ajili ya kuhamasisha suala zima la maendeleo.
 Baadhi 
ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), waandishi 
mbalimbali wa habari pamoja na wamiliki wa mitandao ya kijamii, Blogs, 
wakisikiliza maneno mazuri kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Tanzania, 
Profesa John Nkoma, hayupo pichani. Hii ni sehemu maalumu ya kuonyesha 
kuwa TCRA wanatambua mchango wa mitandao ya kijamii, hususan blogs na 
wamiliki wao kwa ujumla.
Afisa 
Uhusiano wa TCRA,Innocent Mungi akiwakaribisha wadau mbalimbali wa mambo
 ya habari za kwenye mitandao,kuhusiana na uzinduzi wa kampeni ya 
kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano,Warsha hiyo 
imefanyika leo Makao makuu ya Ofisi hizo,zilizopo barabara ya Sam Nujoma
 jijini Dar.
 Wadau wa
 mawasiliano wa mitandao ya kijamii, blogs, wakisikiliza hoja mbalimbali
 zilizotolewa na viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA katika
 uzinduzi wao wa matumizi mazuri ya mitandao kwa ajili ya kuhamasisha 
maendeleo ya Taifa.




1 comment:
Nimeipenda hiyo tupo pamoja
Post a Comment