Monday, July 29, 2013

Mwonekano wa leo wa nyumba za gharama nafuu NHC Mvomero

 Vijana wakiwa kazini kuendelea na ufyatuaji wa matofali eneo la Mvomero Mororgoro , (wa pili kulia mwenye shati la madoa madoa) ni Muungano Kasibi Saguya, Meneja Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa.
Vijana wakiwa kazini kuendelea na ufyatuaji wa matofali eneo la Mvomero Mororgoro ,kwa mbali (kulia) ni Veneranda Seif, Meneja Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Morogoro.
Meneja Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Morogoro, Veneranda Seif, akizungumza na timu kutoka makao makuu iliyokuwa ikipita katika miradi kuangalia shughuli za ujenzi pamoja na ufyatuaji matofali zinazofanyika katika miradi mbalimbali ya gharama nafuu
Kwa mbali inaonekana misingi ya nyumba za gharama nafu za NHC Mvomero ambapo kushoto anaonekana Meneja Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Morogoro, Veneranda Seif, akishuhudia mmoja wa vijana wa Veta waliopata mafunzo kutoka Afrika Kusini akifyatua matofali ya Hydroform.


No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...