Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal Akutana na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam

 Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke, Mhe. Abas Mtemvu, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,jana Julai 6, 2013 kwa ajili ya kuzungumza na wajumbe hao.
 Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakisimama kumkaribisha Mlezi wao katika Ukumbi wa Karimjee, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam,jana Julai 6, 2013. 
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika Ukumbi wa Karimjee wakimsikiliza Mlezi wao, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipozungumza nao.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Comments