Wednesday, July 10, 2013

NHC YAMPIGA TAFU MISS TANZANIA 2012 KUJENGA BWENI LA ALBINO BUHANGIJA

Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (kulia) akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 4.1 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Susan Omari jijini Dar es Salaam jana. Fedha hizo ni kwaajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) linalojengwa katika shule ya Msingi Buhangija mkoani Shinyanga. Fedha hizo ni maalum kwaajili ya kununulia mabati ya kuezekea bweni hilo. Kwa mujibu wa Brigitte zaidi ya Shilingi milioni 60 zinahitajika kukamilisha ujenzi huo.

No comments:

Dkt. Samia: Tumeweka fedha nyingi katika Umwagiliaji kukabili Mabadiliko ya Tabianchi

Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan, amesema katika kufikia azma ya mapinduzi sekta ya kilimo Serikali imechukua hatua ya kufanya uwekezaji mkubwa...