Tuesday, July 16, 2013

Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema na Wabunge Wengine Wanne Wa Chadema Wafanya Maandamano ya Amani kuelekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Jiji la Arusha

Wafuasi wa Chadema wakiandamana kuelekea katika ofisi za Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kwenda kumpongeza kwa kusimamia vizuri uchaguzi wa Madiwani.
Wafuasi wa CHADEMA wakishangilia ushindi katika maandamano ya amani ya madiwani wapya na viongozi kwenda kumpongeza Mkurugenzi wa jiji kwa kusimamia uchaguzi vizuri.
 Lema akiwa na madiwani wapya wakiingia katika jingo la Halmashauri kuonana na Mkurugenzi wa jiji
 Madiwani  wapya waliochaguliwa jana na wabunge wa CHADEMA wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa jiji la Arusha Sipora Liana   jana walipofika ofisini kwake kumpongeza kwa kusimamia vizuri uchaguzi madiwani.
OCD wa Arusha Gilles Mulloto akimisihi Mbunge wa Arusha awatawanye wafuasi wa chama hicho waliokuwa wamekusanyika nje ya jingo la Halmashauri wakiwasubiri viongozi wao waliokuwa wamekwenda kuonana na Mkurugenzi wa jiji kumpongeza kwa kusimamia vizuri uchaguzi wa jana,wafuasi hao na viongozi hao walifanya maandamano ya amani  jana.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (katikati) akizungumza kwenye Ofisi za Halmashauri ya Arusha akiwa na madiwani wapya wa Chadema waliochaguliwa juzi. Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Jeremiah Mpinga (Elerai), Edmund  Kinabo (Themi), Kessy Lewi (Kaloleni) na Rayson Ngowi (Kimandolu).Picha na Ferdinand Shayo na Mwananchi

No comments: