CPA Tawi la Tanzania yaanza maandalizi mkutano wa mwakani

Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya nchi wanachama wa
 Jumuiya ya Madola (CPA) Tawi la Tanzania  Mhe. Mussa Zungu 
Azzan akifungua kikao cha Kamati tandaji pamoja na  Sekretarieti
 jijini Dar es Salaam leo kujadili ushiriki wa Tawi la Tanzania katika 
Mkutano Mkuu wa 44 wa  CPA Kanda ya Afrika utakaofanyika 
Windhoek, Namibia kuanzia tarehe 17-27 Julai, 2013. Kushoto 
kwake ni Mratibu wa CPA Bwana Saidi Yakubu na Kaimu Katibu wa 
CPA Bwana Demetrius Mgalami.
  
 Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 45 wa mwaka 
2014 ambapo Spika wa Bunge la Tanzania ambaye ni Mkamu wa 
Rais wa CPA kwa sasa atachaguliwa kuwa Rais wa
 CPA Kanda ya Afrika.
Mjumbe wa Kamati na Mbunge wa Kilindi Mhe. Beatrice Matumbo
 Shelukindo akichangia wakati wa mjadala.
Wajumbe wa CPA Tawi la Tanzania.Picha na Prosper Minja – Bunge

Comments