Jengo la upasuaji la Hospitali ya wilaya ya Usangi mkoani Kilimanjaro, lililofanyiwa ukarabati na NHC hivi karibuni.
Sehemu ya Hospitali ya wilaya ya Usangi mkoani Kilimanjaro, ambapo jengo lake moja limefanyiwa ukarabati na NHC hivi karibuni.
Meneja Huduma kwa Jamii wa NHC , Muungano Kasibi Saguya (wa kwanza mbele) wakishuhudia wagonjwa katika vitanda vilivyonakshiwa na shuka za Shirika la Nyumba la Taifa, wagonjwa hao wamelazwa katika jengo la upasuaji la Hospitali ya Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, .Meneja Huduma kwa Jamii wa NHC , Muungano Kasibi Saguya (kulia) akiwa ameshikilia mojawapo ya shuka zilizotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa. Jumla ya shuka 160 zilitolewa na Shirika hilo.Kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Dk Gina Kagina
Meneja Huduma kwa Jamii wa NHC , Muungano Kasibi Saguya (kulia) akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa jengo la upasuaji lililokarabatiwa na NHC hivi karibuni.
Wafanyakazi wa NHC wakipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Dk Gina Kagina.
Na
Joyce Anael, Mwanga
SHIRIKA
la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Kilimanjaro, limetumia zaidi ya Sh 16 milioni
kukarabati jengo la upasuaji na na kununua mashuka kwaajili ya Hospitali ya
wilaya ya Usangi mkoani Kilimanjaro, lengo likiwa ni kusaidia jamii kupata
huduma bora za afya.
Akikabidhi
jingo hilo juzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,
Meneja Huduma kwa Jamii, Muungano Saguya, alisema ukarabati huo ni moja ya
mikakati ya SHirika katika kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na rasilimali
za taifa.
Alisema
shirika hilo limekuwa likitoa huduma mbalimbali kwa jamii ikiwemo katika sekta
ya afya na elimu, ambapo misaada iyo inatokana na mapato ya kodi yanayolipwa na
wapangaji wa nyumza za Shirika hilo katika maeneo mbalimbali nchini.
“Namna
pekee ya kuwawezesha Watanzania wasio wapangaji wa nyumba za NHC ni kupitia
msaada kama huu wa leo, Niwapongeze wapangaji wa nyumba za shirika mkoani
Kilimanjaro kwa kubadili mwenendo wao na kuwa walipaji wazuri wa kodi nah ii iwe
kielelezo tosha kuwa Shirika hili letu likiungwa mkono linafanya mambo mengi
yenye manufaa kwa wananchi,”alisema Saguya.
Aidha,
Meneja huyo aliutaka uongozi wa Hospitali ya Usangi, ambayo ndiyo Hospitali ya
Wilaya ya Mwanga kulitunza jengo hilo ili liweze kudumu kwa muda refu kulingana
na thamani iliyotumika katika ukarabati.
Alisema
kutokana na uchakavu uliokuwepo, jengo hilo lilikosa sifa ya kufanyika kwa
huduma ya upasuaji, lakini sasa hospitali hiyo inaweza kujivunia kufanya huduma
hiyo baada ya ukarabati huo.
Meneja
wa NHC mkoa wa Kilimanjaro, Shehe Kombo, alisema mradi wa ukarabati jingo hilo
hususan upauaji ulianza Julai Mosi mwaka huu, ukarabati ambao uligharimu Sh 14
milioni.
Alisema
baada ya ukarabati wa jingo hilo, Shirika la Nyumba lilikaa na kutathmini
changamoto zinzoikabili hospitali hiyo ya wilaya na kutoa msaada mwingine wa
shuka 160 ambazo zimegharimu Sh 2,350,000.
Naye
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Dk Gina Kagina alilishukuru shirika hilo kwa
kuona umuhimu wa kukarabati jingo hilo la upasuaji ambalo lilikuwa na hali
mbaya kabla ya kufanyiwa ukarabati.
Pia
alisema kuwa bado kumekuwapo na changamoto nyingi katika hospitali hiyo ya
wilaya ikiwamo uchakavu wa majengo, hivyo kuliomba shirika hilo kuona umuhimu
wa kurudi katika hospitali hiyo na kutoa msaada mwingine.
No comments:
Post a Comment