Saturday, October 06, 2007

Kelele zetu inabidi zifikie mwisho

INAONEKANA kama vile kuna mwamko fulani miongoni mwetu dhidi ya ufisadi, kwa kila mmoja kuonyesha utaalamu wake wa kuzungumza kadiri awezavyo.

Wengine wameingia mikataba ya kutopokea rushwa wakasaini kwa mbwembwe, na bashasha kubwa lengo likiwa ni hilo hilo.

Wahariri nao wakatia saini kule Ubungo Plaza wakapitisha maazimio, nao wanataka kupambana na ufisadi na wakaapa kabisa kwamba lazima waikomeshe rushwa. Sijui nini kimewatuma sasa badala ya kuanza kuchachamaa kabla.

Kabla ya hapo, nimemsikia mzee wangu Dk Willibrod Slaa akiwaanika hadharani wale aliodai kuwa ni mafisadi wakuu wa nchi hii na hajaishia hapo amebeba ile orodha ya mafisadi na akahama nayo kwenda huko Marekani. Bonyeza hapa upate kusoma uchambuzi huu zaidi.

No comments:

RAIS SAMIA ASHIRIKI NA KUTUNUKU TUZO ZA WASANII WA KOMEDI TANZANIA 2025

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki kama mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wasa...