Sunday, September 11, 2016

RAIS DKT.MAGUFULI AAHIRISHA ZIARA NCHINI ZAMBIA


magRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara ya siku tatu nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe.Edgar Chagwa Lungu ili aweze kushughulikia tatizo la tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16 ,mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa kubomolewa mkoani Kagera.
Kufuatia kuahirisha ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha katika sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe.Edgar Chagwa Lungu
Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.
Jaffar Haniu
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Dar Es Salaam
11 Septemba, 2016

No comments:

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AMWAKILISHA WAZIRI WA FEDHA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA MWAKA LA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI – ARUSHA

Naibu Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Mhandisi Mshamu Ali Munde, amemwakilisha Waziri wa Fedha katika ufunguzi wa Kongamano la 16 la Mwaka la Wa...